Jumapili 17 Agosti 2025 - 17:51
Kampeni ya “Wakati wa Arubaini” Itaendelea Hadi Mwisho wa Mwezi wa Safar

Hawza/ Mazuwari wa Huseini kwa kushiriki katika kampeni ya “Wakati wa Arubaini” wanaweza kulishirikisha Shirika la Habari la Hawza kwa kutuma picha na video za matembezi yao ya Arubaini hadi Jumapili tarehe 2 Shahrivar (sawa na tarehe 30 Safar), ili zichapishwe katika chombo hiki cha habari.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza katika masiku ya Arubaini ya Husein (a.s.) na matembezi ya watu wanaompenda Abā ‘Abdillāh al-Husein (a.s.) kuelekea Karbalā al-Mu‘allā, Shirika la Habari la Hawza limezindua kampeni ya “Wakati wa Arubaini”, kutokana na kuzingatia maombi ya wasomaji na watazamaji, kampeni hii itaendelea hadi mwisho wa mwezi wa Safar.

Mazuwari wa Huseini wanaoshiriki katika kampeni hii wanaweza kutuma picha na video zao za matembezi ya Arubaini hadi Jumapili tarehe 2 Shahrivar (sawa na 30 Safar) kupitia anuani hii: eitaa.com/hozeh_content, ili kushirikishwa na Shirika la Habari la Hawza kwa ajili ya kuchapishwa.

Kwa kazi zilizochaguliwa, zawadi zitatolewa kwa njia ya bahati nasibu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha